Please enter CoinGecko Free Api Key to get this plugin works.
MUHTASAR.
ili tuweze kupata mafanikio siku zote ni lazima tujitaarishe kisaikolojia ili tuweze kujua hasa tunachokitafuta na tuweze kuwa na mtazamo (focus) kubwa ya juu ya kile tunachokitaka.
walio wengi wanapoanza jambo fulani huwa wanaanza kwa malengo lakini baada ya kuanza tu mitazamo yao huwa inaanza kubadilika na hatimae wanapoteza dira ya kile wanachokitafuta na kuishia patupu. kwaiyo ni lazima ujifunze haya na uyazingatie kwa asilimia zote 100% kabla ya kuanza kufanya chochote katika kozi hii ili nawewe usije ukapoteza lengo kama wanavopoteza watu wengine.
hakuna kitu rahisi kwenye maisha hususwani kwenye jambo la mafanikio. ila urahisi unakuja baada ya wewe kuamua kwa moyo mmoja kujifunza na kuyafanyia kazi yale unayojifunza kila siku. ukifanya ivo ndipo utaanza kupata mabadiliko na kutakupelekea kutofautiana na watu wengine ambao wao wanajifunza lakini hawayafanyii kazi yale wanayojifunza na kupelekea kutokubadilika maisha yao na kubaki vile vile hadi leo hii.
hakikisha hapa unajifunza kwa faida. na ili upate faida basi hakikisha unakuwa bega kwa bega kwa yale yote unayoyapata hapa. mungu akipenda hakika baada ya kujifunza kipengele hiki cha SAIKOLOJIA YA MAFANIKIO basi utaanza kuwa mtu mpya kabisa, mwenye maono ya mbali na mwenye kujua hatua zote unazopaswa kufanya ili upate mafanikio ya haraka. tuwende kazi sasa…